
![]() |
Picha ikionesha maji yanavyotiririshwa kwenye maeneo yanayotumiwa na wananchi. |
![]() |
Picha juu na chini, ni Chemba ya maji machafu inayomwaga maji kayika maeneo ya wakaazi. |
Baadhi ya wananchi na
wafanyabiashara wanaopita na kufanya kazi zao katika mtaa wa barabara kuu mjini
Dodoma, wamelalamikia ofisi za makao makuu ya chama cha Mapinduzi(CCM) mjini
humo, kutiririsha maji yenye kinyesi barabarani.
Wananchi hao wamesema kuwa tatizo
hilo ni kero kwao kwani licha ya harufu mbaya inayosambaa katika maeneo yao,
bado wanahofia mlipuko wa magonjwa kutokana na uchafu huo uliokithiri.
Mkazi mmoja wa mtaa wa Kinyonga
ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema kuwa wanashangazwa na kitendo cha
Ofisi ya Chama Tawala nchini, kushindwa kudhibiti hali hiyo licha ya kuwa CCM
ndiyo chama tawala, hapo ni makao makuu.
“Mwandishi hili swala mi naona ni
uzembe tu,maana hawa ndiyo wanaoshikilia dola,na hawa ndiyo serikali sasa
kitendo cha kuacha maji taka kutitirika barabarani ni kama kutojali,wao hawaoni
kero maana kila kukicha wapo juu ya mashangingi yao ila sisi tunaotumia
barabara kwa miguu kila kukicha ndo tunajua hii adha,” Alisema mkazi huyo.
Mfanyakazi mmoja wa Serikali mjini Dodoma,
aliyejitambulisha kama P, amesema kuwa kitendo hicho ni aibu kwa mji kama
Dodoma,mji ambao ni sebure ya nchi, na kwamba uchafu huo unaupa sifa mbaya mji
huo.
“Hapa Dodoma ni sebure ya nchi maana
Mawaziri,Wabunge na viongozi wakubwa wanapita na wengine wanaishi hapa, lakini
wanashindwa kunyonya maji kwenye chemba,hii ni aibu kwa mji na nchi kwa ujumla.’’Alisema
P.
Inaonekana maji taka hayo husambaa
katika barabara Kuu na kutoa harufu kali hususani nyakati za jioni na asubuhi.
Jitihada za kuwapata wahusika wa
ofisi za makao makuu ya chama cha Mapinduzi mjini Dodoma zinaendela, ili kujua
hatma ya kero hiyo katika eneo hilo,kwani mwandishi amefika katika ofisi hizo
asubuhi ya leo na kushindwa kumpata mzungumzaji, kwa mujibu wa utaratibu wa
ofisi hiyo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment