MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday, 13 August 2014

NEWS ALERT!!! BABA ASKOFU KILAINI & MBUNGE KHAMIS KAGASHEKI, HAKUNA KUPELEKA WANAFUNZI NJE YA NCHI;

 Katika uzinduzi huo, mgeni rasmi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Bukoba mjini kupitia CCM balozi Khamis Kagasheki, amesema uwekezeji katika elimu si jambo la kubeza, na kuongeza kuwa wawekezaji wawe na moyo wa kusaidia, wasiwekeze kwa lengo la kujipatia pesa pekee, huku akiongeza kuwa kama mbunge wa jimbo hilo, na chuo kipo jimboni mwake, yuko tayari kutoa ushirikiano kwa nguvu zote hasa katika suala hili muhimu la elimu, ili wazazi na walezi wasiangaike kupeleka watoto wao nje ya nchi.

Askofu msaidizi wa jimbo katoliki la Bukoba, Baba Askofu Method Kilaini, amesema kuwa kupeleka watoto nje ya nchi ni aibu, kwani inatokana na kukosa shule na vyuo bora mkoani humo, kwani wawekezaji wengi wamekuwa na nia ya kujipatia pesa na kuoa elimu isiyo na kiwango cha kuwasaidia wanafunzi, hivyo wazazi wanaamua kupeleka watoto nje ya nchi na kubakiza jina la NSHOMILE, kwa maana ya kujua kusoma na kuandika pekee.
Mmiliki wa chuo cha ERA wa kwanza kushoto na mgeni rasmi katika uzinduzi huo Balozi Kahamis Kagasheki MB mwenye tai.
Picha juu na chini, ni wanafunzi wanaosoma chuoni ERA, wavulana kwa wasichana.

Chuo cha ualimu ERA, kinatoa mafunzo kwa ngazi ya cheti na dploma, kipo Bukoba mjini katika kata ya Kitendaguro kilomita 5 kutoka katikati ya mji.
Na Mwanaharakati.

No comments: