Taarifa kutoka idara ya ulinzi ya
Marekani Pentagon zinasema kuwa mmoja wa wanzilishi wa kundi la Al Shabaab
Ahmed Godane ameuawa.
Marekani imesema kuwa kuuawa kwa
Godane ni hatua kubwa sana katika harakati dhidi ya wapiganaji hao wamekuwa
msumari mkali kwa mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki na hata kwa serikali ya
Somalia yenyewe.
Katibu wa Pentagon Nchini Rear Admiral
John Kirby ametangaza kuwa Ahmed Godane ameuawa katika oparesheni iliyofanywa
nchini Somalia Jumatatu wiki hii.
Kwa Mujibu wa Admiral Kirby, kuuawa
kwa Godane ni pigo kubwa zaidi kwa kundi hilo la Al shabaab na itasaidia
kukabiliana na ugaidi unaofanywa na kundi hilo eneo la Afrika Mashariki.
Marekani imekuwa ikishirikiana na
washirika wake wakuu kukabili wapiganaji hao wa AL shabaab ambapo katika miaka
ya hivi karibuni wamezidisha mashambulio sio tu nchini Somalia bali hadi nchi
jirani.
Wiki iliyopita Kikosi cha kulinda
amani chini ya mwavuli wa Muungano wa Afrika AMISOM kikishirikiana na majeshi
ya serikali ya Somalia kilianzisha oparesheni kali kuwasaka wapiganaji hao wa
AL shabaab. Na kufikia mwanzoni mwa wiki hii Marekani ikajiunga katika oparesheni
hiyo ambapo walishambulia msafara ambao Ahmed Godane alishukiwa kuwa ndani.
Walioshuhudia waliambia waandishi
habari kuwa muda mfupi baada ya msafara huo kushambuliwa, ndege za kivita za
helikopta zinazoaminiwa kuwa za Marekani zilishuka na kubeba maiti zote zilizo
kuwepo.
Kwa hiyo kwa muda hakukuwa na thibitisho lolote iwapo Godane mwenyewe
aliuawa au la.
Upande wa AL shabaab nao walianza
kukusanya watu katika kijiji karibu na eneo hilo la Shebeele ambako shambulio
lilifanywa na kuwaua au kuwateka wengijne ambao hadi sasa hawajulikani waliko.
AL shabaab hawakuzungumzia iwapo
Godane alikuwa miongoni mwa waliouawa.
Leo asubuhi kulikuwa na picha zilizo
sambazwa katika mtandao ambazo hazikuthibitishwa zilizodai kuwa ni Ahmed Godane
bado alikuwa hai.
Al shabaab hawajasema lolote baada
ya tangazo la Pentagon kuthibitisha kifo cha Godane
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment