Mwenyekiti
wa NEC Jaji Mstaafu Damian Lubuva, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam na
kufafanua kuwa kutolewa kwa fedha hizo kutaiwezesha tume hiyo kuanza mara moja
uboreshaji wa daftari hilo, zoezi lililochelewa kwa zaidi ya mwezi mmoja
kutokana na kutokwepo kwa fedha.
Kuidhinishwa
kwa fedha hizo kumekuja licha ya wadau viiwemo vyama vya siasa, kuhoji wapi
tume ya uchaguzi itazipata fedha hizo, kutokana na bajeti iliyotengwa na bunge
kwa ajili ya utendaji wa ofisi hiyo kuwa ni zaidi ya mara kumi ya kiwango
kilichopangwa kutumika kwenye uboreshaji daftari la wapiga kura.
Mmoja
wa wadau waliolalamikia fedha hizo ni Mwenyekiti wa Chama cha upinzani cha CUF
Profesa Ibrahim Lipumba ambaye amesema inashangaza kuona serikali inapanga
matumizi ya fedha ambayo hayajaidhinishwa na bunge.
Aidha,
Profesa Lipumba ameongeza kuwa hata teknolojia itakayotumiwa kwenye daftari
hilo ina mapungufu mengi kwani tofauti na inavyoelezwa kuwa itafanya uhakiki na
utambuzi wa wapiga kura kuwa rahisi, teknolojia hiyo imeonyesha mapungufu
makubwa kwenye nchi ilikotumika ikiwemo nchi za Kenya na Malawi.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment