
Wakiwa
katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru walikopelekwa kwa matibabu na
kuangaliwa maambukizi ya magonjwa ya zinaa, watoto hao walidai kufanyiwa mchezo
huo kwa nyakati tofauti na wachungaji watatu wa kanisa hilo lililopo eneo
la Feed Force, Kwamrombo jijini Arusha.
Mmoja
wa watoto hao anayesoma darasa la 4 katika shule ya msingi alieleza kuwa yeye
na wenzake wamekuwa wakifanyiwa mchezo mchafu katika kanisa hilo baada ya
wachungaji hao kuwapatia shilingi 2,000 za kufungia mdomo.
“Siku moja nilipofika shuleni wenzangu wakaniambia
niende pale kanisani tukapewe hela, nilipofika niliwaona wenzangu wengine
wakifanyiwa mchezo mchafu na mimi mchungaji aliniambia niiname akanifanyia
kitendo kibaya na kunipa shilingi 2,000, niliumia sana,’’ alisema
mwanafunzi mmoja.
Mwanafunzi
mwingine alisema amekuwa akitoroka shuleni na wenzake na kwenda kwa watumishi
hao ambapo huwaingiza katika kanisa hilo na kujifanya wanawaombea baadaye
huwafanyia mchezo mbaya.
“Tukifika huwa wanatufungia ndani na kutuambia
tuwanyonye, baadaye wanatubaka na wakimaliza wanatuambia tukisema kwa mtu
yeyote watatuchinja na kutuzika ndani ya kanisa lao,” alisema
denti huyo.
Wanafunzi
hao walieleza kuwa watumishi hao huwarubuni kwa kuwaeleza kuwa watawasaidia
kuwasomesha iwapo watakuwa wakienda kwenye kanisa hilo na kuwaingilia.
Mzazi
mmoja wa watoto hao, Julius, mkazi wa Kwamorombo alisema mtoto wake alimweleza
kwamba amekuwa akifanyiwa mchezo mbaya na watumishi hao baada ya kupewa
shilingi 2,000.
Alisema
aligundua hilo kufuatia tabia ya mtoto wake kuchelewa kurudi nyumbani.
Naye
Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless Lema ambaye alifika
hospitalini kuwajulia hali watoto hao alisikitishwa na kitendo hicho na
kulitaka jeshi la polisi lifanye uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na vipimo
vya kidaktari ili kupata ukweli wa tukio hilo.
“Nimeongea na mkuu wa mkoa, Magesa Mulongo ambaye
ameahidi kulifuatilia kwa kina suala hili na kujua undani wake,’’ alisema
Lema.
Hata
hivyo, watoto hao baadaye walihamishiwa katika Hospitali ya Seliani kwa ajili
ya vipimo zaidi huku taarifa za awali zikithibitishwa na daktari wa hospitali
hiyo kuwa, baadhi yao walikutwa na michubuko na kupanuka sehemu za siri hali
inayooneshwa kuingiliwa.
Watuhumiwa
wa tukio hilo wanashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Arusha kwa
uchunguzi zaidi na Kamanda wa Polisi Arusha, Leberatus Sabas amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment