Taarifa ilioufikia mtandao huuu muda mfupi uliopita, inasema kuwa shughuli za wananchi zimesimama katika maeneo kadhaa ya jiji la Arusha, huku baadhi ya wananchi wakishindwa kufungua nyumba zao kwa kuhofia usalama wao baada ya kusikia miungurumo ya ndege za kivita kutanga katika anga la jiji hilo, huku magari ya kijeshi yakipita katikati ya mji yamebeba vifaru.
Tetesi zinasema kuwa jeshi la Tanzania kupitia kikosi cha Monduli Arusha, ndege hizo zingine hazina rubani ndani yake na ziko kwenye mazoezi ya kawaida, hivyo watanzania wasiwe na wasiwasi na ndege hizo.
Tuna mtafuta kamanda wa polisi jijini Arusha Liberatus Sabas kwa taarifa zaidi.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment