Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la
Iraq na Syria (ISIS) limetekeleza mauji mengine ya kutisha kwa kumkata kichwa
mwandishi mwingine wa habari wa Marekani.
Mwandishi huyo aliyetajwa kwa jina
la Steven Sotloff mwenye umri wa miaka 31
alitekwa na wapiganaji hao mwezi August mwaka jana.Mwezi uliopita Sotloff
alionekana mwishoni katika picha za video zilizoonyeshwa kuhusiana na kuchinjwa
kwa mwandishi mwingine wa Marekani James Foley.
Katika video hiyo iliyopachikwa
hapo chini, mwandishi huyu anaonekana kuuawa na mtu anayemruhusu
kutoa semi yake ya mwisho.
Sotloff ambaye katika video hiyo amevalia magwanda ya rangi ya chungwa akiwa amepiga magoti anasikika akisema kuwa:
'Obama, your foreign policy of intervention in Iraq was supposed to be for preservation of American lives and interests, so why is it that I am paying the price of your interference with my life?.''
Mpiganaji mmoja wa kundi hilo
akizungumza kwa kiingereza anamlaumu Rais Obama kwa kifo cha
mwandishi habari huyo.
“I’m
back, Obama, and I’m back because of your arrogant foreign policy towards the
Islamic State..
“As your missiles continue to strike our people, our knife will continue to strike necks of your people,” anasikika akisema kabla ya kutekeleza kitendo hicho cha kikatali.
Muuaji huyu anasadikika kuwa ni yule yule aliyemchinja mwandishi wa kwanza mwezi uliopita.
“As your missiles continue to strike our people, our knife will continue to strike necks of your people,” anasikika akisema kabla ya kutekeleza kitendo hicho cha kikatali.
Muuaji huyu anasadikika kuwa ni yule yule aliyemchinja mwandishi wa kwanza mwezi uliopita.
Punde baada ya kukamilisha hotuba
yake,muuaji huyo anaanza kumchinja Sotloff lakini video hiyo inazimwa .
Sekunde chache baadaye mateka
mwingine raia wa Uingereza David Cawthorne Haines, anaonekana
kabla ya ilani kutolewa kuwa hatima yake iko mikononi mwa taifa la Marekani.
Na Mwanaharakati.


No comments:
Post a Comment