MKUU wa kituo cha polisi cha
Nyamboge kilichopo katika kata ya Katoma Wilayani Geita Mkoani hapa amenusulika
kupigwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kukutwa akitaka
kufanya mapenzi na mwanafunzi katika nyumba anayoishi mwanafunzi huyo.
Tukio hilo limetokea jana majira ya
saa tatu usiku ambapo wananchi wa kijiji hicho wakiwa na marungu na mikuki
waliweka mtego wa kumnasa mkuu huyo aliyefahamika kwa jina Moja la Venance
kuwa ana tabia za kumrubuni mwanafunzi huyo kwa mda mrefu.
Aidha akizungumzia tukio hilo binti
huyo Rozimery Kahindi (17) anayesadikiwa kuwa mwanafunzi wa kidato cha
nne alisema kuwa siku ya jumapili, mkuu huyo wa kituo alituma maaskari wawili
wakaenda kumkamata huku akidai kuwa hajui hata kosa lake, lakini akalazimika
kwenda na alipofika hapo alianza kulazimishwa kuwa anatembea na mwalimu wake,
ndipo alipokataa na kulazimishwa kuandika maelezo ambayo hata yeye hayakumbuki
hadi anakutana na wanahabari.
Aliendelea kusema kuwa baada ya
kukataa kuandika maelezo alipelekwa rokapu na mda mfupi alifuatwa na askari
mmoja kati ya wale waliomkmata kuanza kuandika maneno ya kutoa kichwani mwake
na kulazimsha kusaini lakini aliendelea kugoma na alipigwa sana na kuamua
kusaini kutokana na kutishiwa kufungwa na mara baada ya kusaini aliitwa na OCS
huyo na kumwambia aende Nyumbani lakini arudi jioni ana shida naye ya muhimu
sana lakini alaishindwa kurudi kutokana na kuchoka na kipigo alichokipata
kituoni hapo.
Kutokana na mkuu huyo wa kituo
kutuhumiwa na mwanafunzi kuwa anamtaka kimapenzi ilibidi awaambie wanafunzi
wenzake na wananchi na baada ya hapo wakatengeneza mtego ili wamnase.
Siku ya jumapili jana mkuu huyo wa
kituo alikwenda Nyumbani kwa mwanafunzi huyo na kuomba wafanye mapenzi kwa kuwa
wenzake anaoishi nao hawakuwepo lakini aligoma kufanya hivyo, ndipo muda mfupi
wananchi waliokuwa wamemuona anaenda kwa binti huyo walifika hapo
na kufunga mlango kwa nje na kuanza kupiga kelele na kumfanya OCS huyo kuvunja
malango na kutoka nje lakini wanchi walifanikiwa kumkamta na kuanza kumpiga
ambapo aliokolewa na askari na kufikishwa katika kituo kikuu cha
polisi cha Wilaya ya Geita.
Diwani wa kata hiyo Josephat Komanya
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kulaani vikali kitendo
hicho na kuwaomba wanafunzi wa kata hiyo kuendelea kuwataja viongozi ambao
wanawataka kimapenzi kwa nguvu.
Jitiada za kuzungumza na kamanda wa
jeshi la polisi Mkoni hapa Joseph Konyo zinaendelea.
Na.Valence,Robert,Geita.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment