WATU wawili wamekufa kwa kugongwa na
trekta katika kijiji cha Mtakata kata ya Magamba wilayani Mlele mkoani Katavi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi
Kamishina mwandamizi msaidizi Dhahiri Kidavashari aliwataja waliokufa kwenye
ajali hiyo kuwa ni Ramadhan Shaban (20) mwanakijiji wa Kapanda wilaya na Alex
Lucas (Makanyanga) mwanakijiji wa Kashaulili mjini Mpanda.
Alisema ajali hiyo ilitokea saa 2 usiku katika kijiji cha Mtakata wilayani Mlele huku
akibainisha kwamba marehemu hao walikuwa kwenye pikipiki yenye namba za usajili
T481 CVE aina ya Boxer iliyokuwa ikiendeshwa na Ramadhan wakitoka kijiji cha
Kapanga.
Kamanda Kidavashari alisema trekta
iliyowagonga ni namba T347 BXV aina ya Tafe lililokuwa likiendeshwa na mtu
asiyefahamika huku akibainisha kwamba chanzo cha ajali hiyo ni trekta hilo kuwa
na taa moja.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment