Taarifa inasema kuwa ndugu wa marehemu Said Francis
na Issa Yusuph walifika katika eneo la makaburi, na kukuta mwili wa marehemu
umefukuliwa na kuachwa juu ya kaburi.
Baada ya kufanyika uchunguzi na madaktari katika
mwili huo, wamesema kuwa hakuna kiungo kilichoondolewa, na kuwafanya wananchi
kuwa na hisia za imani za kishirikina.
Imam wa msgid Twaqua Musoma Suleiman Khamis akatoa
taarifa kwa mashuuda kuwa ni la kishirikina inabidi walaaniwe kwasababu adhabu
yao mungu amewaandalia kwani wamekata ubao alipokuwa amehifadhiwa
marehemu(MWANANDANI).
Naye mchungaji Dk Mozes Zephania kutoka kanisa la
Evangelist assemblies of God amesema binadamu inabidi kumrudia Mungu ili kuacha
matukio kama hayo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment