Katika hali isiyotarajiwa,
mwanafunzi wa Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo
Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Ezra Gerald (19), amejinyonga hadi kufa kwa
kutumia shuka hospitalini, alikokuwa amelazwa kwa kinachoeleza alikuwa
anasumbuliwa na homa ya matumbo.
Hata hivyo, ujumbe ulioachwa na
marehemu huyo unaonesha alichukua uamuzi huo, kutokana na kuchukizwa na uamuzi
wa daktari aliyemhudumia wa kumlaza ili atibiwe bila kufanyiwa vipimo sahihi.
Tukio hilo limethibitishwa na Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Gilles Muroto aliyesema mwanafunzi huyo
alijinyonga Septemba 16 mwaka huu saa moja asubuhi.
Alisema mwili wake uligundulika
ukining’inia kwenye mti uliopo maeneo ya hospitali hiyo na alipopekuliwa katika
mifuko ya suruali yake, zilionekana karatasi mbili, moja ikiwa na ujumbe
uliosomeka; “Haiwezekani binadamu kuhudumiwa kama mbwa, yaani nafika
hospitali najieleza hali yangu halafu daktari ananiandikia kulazwa bila kupima,
sasa sijui wanatibu nini?
“Kwa kweli siwezi kuvumilia wenzangu
wanasoma halafu mimi nimekalishwa tu hapa hospitali bila kujua wananitibu nini,
inaniuma sana mpaka nafikia hatua hii ya kujiondoa duniani kwa sababu naona
watu wanachezea ndoto zangu, mimi siwezi kuona ndoto yangu inazimwa wakati
natakiwa niwepo shuleni nikamilishe ndoto zangu “mjitahidi tukutane mbinguni
“Respect My Family and Brother Henry.”
Kamanda Muroto amesema hakuna
aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo, lakini polisi wanaendelea na uchunguzi.
Inaelezwa mwanafunzi huyo aliyetajwa
kuwa ni mwenyeji wa mkoa wa Tabora, alilazwa hospitalini hapo tangu Septemba 11
mwaka huu.
Kwa mujibu wa Katibu wa Hospitali ya
Mkoa wa Kagera, Benges Justus, tukio hilo lilitokea Septemba 16, mwaka huu,
siku moja baada ya mgonjwa huyo kulazwa.
Alisema baada ya mwanafunzi huyo
kupokelewa hospitalini hapo, alifanyiwa vipimo vyote vya kitabibu na
kugundulika anasumbuliwa na malaria, ndipo akaanzishiwa tiba ya ugonjwa huo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment