WADAU wa rasilimali za uvuvi
wilayani Muleba mkoani Kagera wamechanga kiasi cha Sh 40 mil kwa ajili ya
kununua boti yenye mwendo kasi itakayotumika kukabiliana na vitendo vya
ujambazi wa wavuvi ndani ya ziwa victoria.
Fedha hizo zimechangwa jana
wilayani humo katika harambee iliyoongozwa na mkuu wa mkoa wa kagera
kanali mstaafu Fabian Masawe na malengo ya wadau hao ni kukamilisha
Shilingi milioni 72 zinazohitajika kununua boti hiyo
Akisoma risala kwa wadau hao diwani
wa kata ya Mazinga Bw Alex Thadeo amesema matukio ya ujambazi kwa wavuvi
wilayani Muleba yamewaathiri na mashine za uvuvi 65 zenye thamani
ya Sh292.5mil zimeporwa mwaka huu
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi wilayani Muleba Bw Muhaji Bushako amelalamikia watumishi wa
Marine na Sumatra mkoani Kagera kwa kuhujumu nguvu za wavuvi wanapoingia
visiwani bila wilaya kuwa na taarifa
Hata hivyo mkuu wa mkoa wa kagera
Kanali mstaafu Fabian Masawe amewataka wavuvi kwa kushirikiana na vyombo vya
dola kudhibiti vitendo vya uvuvi haramu ili kuhakikisha samaki
wanaovuliwa wanakuwa ni wenye soko kiuchumi.
Aidha amewaahidi wavuvi hao
kuwapatia askari wa doria kutoka jeshi la polisi ambao watakuwa na mafunzo ya
kutumia slaha kali kupambana na waharifu wanaovamia ziwani na kupora zana za
uvuvi huku wakiacha madhara makubwa
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment