
Waamini
mkoani Kagera wameshauriwa kuwa makini wanapokuwa wanatamka maneno katika jamii
ili kutunza amani na ulivu uliopo katika nchi yetu.
Kauli
hiyo imetolewa na mchungaji wa usharika wa kanisa la kiinjili la kirutheli tanzania
Kashura dayosisi ya kasikazini magharibi Alex Kasisi wakati akiongoza ibada
maalum ya changizo la ukarabati wa kanisa hilo leo.
Mchungaji
Kasisi amesema kuwa,ndoa nyingi zinazovinjika mara nyingi sababu inakuwa ni
matumizi mabaya ya ulimi.
Katika
haranbee hiyo Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Mheshimiwa Balozi Hamis Kagasheki pichani juu, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dokta
REGNALD MENGI ametoa shilingi milioni kumi ikiwa ni kuunga mkono jitihada za waamini
katika ukarabati wa kanisa hilo kongwe la usharika..
Aidha
katika harambee hiyo zimepatika shilingi milioni 22.9 ikiwa ni pesa taslimu na
ahadi zilizotolewa na waamini na watu walioharikwa.
Ukarabati
wa kanisa hilo la Usharika wa kashura utagharimu
shilingi milioni 15.2.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment