Akizungumza mbele ya mgeni rasmi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Bukoba mjini CCM Balozi Khamis Kagasheki, katika mahafali ya tano ya kidato cha nne katika shule inayomilikiwa na KKKT ya Bweranyange, askofu Bagonza amemwomba mbunge huyo kumsaidia kukamilisha usajili wao ili wasikwame kufundisha katika shule za kanisa hilo kunusuru wanafunzi wa sayansi.
Amesema kuwa alienda Sri Lanka kufanya mazungumzo, na kukubaliana na walimu kadhaa ambao kwa mujibu wake anataka kubadilisha mawazo na mtazamo wa elimu ya tanzania kupitia walimu kutoka nje, huku akisema kuwa walimu wa ndani waache kushinikiza mishaara mikubwa, kisa wanafundisha sayansi.
Katika mhafali hayo, wanafunzi 67 wa kike wamehitimu kidato cha nne, huku shule hiyo ikikabiliwa na mapungufu ya kompyuta, huduma ya maji na umeme, ambavyo mh. Kagasheki amesema ankwenda kuzungumza na rafiki zake, ili kuona jinsi ya kusaidia vitu hivyo, huku akiomba apewe bajeti yake.
|
Balozi Kagasheki, akifanyiwa utabiri na mwanafunzi kutaja na ni kitu gani ameshika mkononi wakati wa mchezo wa kuigiza.. |
|
Mgeni rasmi katika mahafali hayo Balozi Kagasheki akikabidhi cheti kwa moja ya mwanafunzi muhitim. |
|
Askofu Bagonza kushoto, akiongozana na Balozi Kagasheki katika ukaguzi wa mazingira ya shule hiyo ya wanafunzi wa kike,ambapo hatahivyo balozi ameoneshwa maabara ya shule hiyo inavyofanya kazi. |
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment