MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday 29 September 2014

NEWS ALERT!!! TIZEBA ELIMU LAZIMA IZINGATIWE



NAIBU  waziri  wa mawasiliano na uchukuzi  Dk  Charles Tizeba  ambaye  pia  ni mbunge wa jimbo la Buchosa Wilayani Sengerema mkoani Mwanza amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii kwa kuwa elimu ndiyo urithi pekee.
Dk  Tizeba  ametoa  wito  huo  juzi katika  kata  ya  Nyehunge  wakati akikabidhi msaada wa vitabu elfu moja vya somo la Hisabati kwa walimu wakuu wa shule kumi na nane za sekondari katika jimbo la Buchosa.

Amesema  kuwa  lengo  la  kugawa  vitabu  hivyo  katika  shule  hizo  ni kuasaidia tatizo la upungufu wa vitabu mashuleni na kuwawezeasha wanafunzi kujisomea vizuri na hatimaye waweze kufanya vizuri katika mitiahani ya ya taifa.
 .
Dk  Tizeba  aliongeza  kuwa  vitabu    hivyo  vya  somo  la  hisabati ni kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili na kwamba vimegharimu shilingi milioni 9.

 Aidha  amewataka  walimu  wakuu  wa  shule  za  sekendari  jimboni  humo kuakikisha vitabu hivyo vinatunzwa kwa uangalifu mkubwa na umakini zaid.

 Mwalimu  mkuu  wa  shule  ya  sekondar Nyehunge  Rubhari
Benesta akisoma  risala  fupi  kwa  mbunge  wa jimbo  hilo
alisema   kuwa  wanafunzi  wa  shule  za  sekondari  katika  jimbo
wanaotoka  mbali  na  maeneo  ya  shule hizo wanaishi  katika
mazingira magumu ya upangaji kutokana na shule kutokuwa na hostel.
 
Naye afisa  elimu  vifaa na  takwimu  shule za  msingi
Wilayani  sengerem  Pius  Lwamimi  akishukuru  kwa  niaba ya  ofisa elimu idala ya sekondari Wilayani sengelema ameongeza DK Tizeba kwa msaada wa vitabu hivyo na kuwaomba wengine kuiga mfano huo.


Na Mwanaharakati.

No comments: