MGAMBO wa kituo cha
polisi cha Nzera kilichopo Tarafa ya Bugando Wilayani Geita Mkoa wa Geita
wanatuhumiwa kumshambulia kwa kipigo mwalimu msitaafu kisha kumvunja mbavu zake
bila kukamatwa
Kufuatia hali hiyo
wananchi wa kijiji cha Nyamboge Katika kata ya Katoma Wilayani Geita
Mkoani hapa wamelituhumu Jeshi la polis Mkoani hapa kwa kushindwa
kumkamata mtuhumiwa aliyeusika kumpiga Samsoni Mzingwa(58) na kumvunja
mbavu zote na huku aliyefanya kitendo hicho hakiwa mitahani hakitamba
na kujigamba kuwa polis wemewekwa mfukoni mwake.
Tukio hilo limetokea
tarehe 14 mwaka huu majira ya asubuhi wakati Mwalimu Samsoni
Mzingwa(58),akielekea shambani kwake.
Akizungumza kwa shida
Samsoni alisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni yeye alikodiswa shamba
mwezi huu kwa ajili ya la kulima Maindi na Rukasi Bunzali pamoja na
Wiliamu Bunzali wote wakiwa ni wanafamilia moja kwa makubaliano ya kuwalipa
miliono moja na laki tanona kulipa pesa zote na kuanza kulima mala moja
kwa ajili ya kupanda mazao yakiwemo maindi na mahalage.
Lakini juzi wakati
akienda shambani kwake alishutukia watu wanne wakiwa na mgambo wawili wa kituo
cha polis Nzera kilichopo katika wilaya Geita wanamzingila na kuanza kushushia
kipigo kikubwa hadi kumvuja mbavu huku wakimtembeza uchi wa mnyama ali
iliosababisha maumivu makali na kulazimika kulazwa katika Hospitali ya wilaya
ya Geita.
Alisema kuwa pamoja na
kuwatambua waliomfanyia kitendo hicho na kuwataja kwa majina kuwa ni Masalu
Mwnangwa na Kona Mwanangwa lakini wamewakamata mgambo na kona wakati Masalu
akizidi kutamba mitaani na huku polis wakiwa wanamuona lakini awataki kumkamata
uenda wanamuogopa kwa kuwa ana pesa alisema Samson.
Naye Mtoto wa Mzee huyo
aliyejitambulisha kwa jina la Baraka Samsoni alisema kuwa kuwa yeye alipata
taalifa na kwenda kulipoti kwa OCS Nzera lakini akuna kilichofanyika zaidi ya
kuzunguswa na OCS huyo huku akiambiwa asiwafundishe kazi asikali hao.
Mganga mfawidhi wa
Hoaptali ya Wilaya ya Geita Adam Sijaona amekili kumpokea mgonjwa na kumalaza
wodi No 8 na kusema baada ya kupiga Picha waliona wanasubili majibu
lakini vipimo vya awali vinaonyesha ameumia mbavu.
Kamanada wa Jeshi la
polis Mkoani hapa Josefu Konyo alipopigiwa sm yake ya mkononi na mwandishi wa
habali hizi na kutaka kujua kwanini awajamkamata mtuhumiwa alikata na
alipotumiwa ujumbe mfupi zaidi ya mala mbili akujibu
Na VALENCE
ROBERT,GEITA
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment