Kauli hiyo imetolewa juzi na Mwenyekiti CCM Mkoa wa Geita
Josefu Msukuma mbele ya Naibu waziri wa nishati na madini wakati akikabidhi
eneo la kuchimba dhahabu kwa wachimbaji wadogo wadogo lililoko katika kijiji
cha Lwamgasa Wilayani Geita mkoani humo.
Msukuma alisema kuwa kumekuwa watu ambao si waungwana
wanaopora maenaeo ya wachimabaji wadogo wadogo kwa kuwalazimisha kuingia ubia
na mwishowe wazudhulumiwa na kuwafukuza ambapo huanza kuhangaika.
Aliendelea kusema kuwa migogoro ya wachimbaji wakubwa na
wadogo haiwezi kuisha kama wachimbaji wakubwa hawataacha kuwadhulumu maeneo yao
hivyo kumuomba naibu waziri kuwachukulia hatua kali wote waliopora maeneo
yaliyotengwa kwa wachimbaji wadogo wadogo na kujimilikisha wao.
Naye Naibu waziri wa nishati na madini akiongea na wananchi
wakati wa kuzindua mgodi huo aliishukuru benki ya dunia na Mgodi wa GGM kwa
kukubali kutoa pesa nyingi na vifaa kwa kuwasaidia wananchi hao mara baada ya
kutambua mahusiano mazuri yaliopo kati ya mgodi na Serikali.
Vilevile aliwataka wananchi wa kijiji hicho pamoja na
Serikali ya mkoa huo kusimamia vizuri mradi huo ili uwezi kuwaendeleza wakazi
wa mkoa mzima kwa kuwanufaisha wao.
Mkurugenzi wa Geita Gold Mine Michael Anen alisema kuwa
wataendelea kuwasaidia wanachi wa mkoa wa Geita kwa kuwa ni mahusiano mazuri
yaliopo kati yao na Mgodi huo ambapo wanarudisha faida yao wanayoipata kwa
wananchi wao.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment