Taarifa ya hivi punde kupitia moja ya redio hapa nchini, inasema kuwa Jeshi la polisi mkoani Arusha limemuua kwa kumpiga risasi mtuhumiwa namba moja wa milipuko ya mabomu katika mikusanyiko na kuwamwagia viongozi wa dini tindikali, baada ya kujaribu kutoroka akiwa chini ya ulinzi njiani kwenda kuonyesha bomu alilokuwa amelificha maeneo ya kondoa mkoani Dodoma .
Taarifa
iliyonifikia memtaja mtuhumiwa huyo anayetajwa kuwa namba moja wa kesi ya
ulipuaji mabomu jijini Arusha, kuwa ni Yahaya Hassan Omar kwa kupigwa risasi na
askari wa jeshi la polisi wakati alipojaribu kutoroka akiwa chini ya ulinzi.
Mtuhumiwa huyo, ameuawa zikiwa zimepita siku chache baada ya kuuawa kwa mtu mmojamkoani Arusha aliyekuwa akituhumiwa kuwateka na kuwauawa wananwake mbalimbali mkoani humo
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment