 |
Ili ndio eneo halisi ndani ya kanisa walipokatiwa mapanga watu hao. |
Taarifa ya awali alizotoa mchungaji wa kanisa hilo ambaye
amejitambulisha kuwa ni
FAUSTINE JOSEPH, amesema
kuwa usiku saa 5, yeye alimaliza ibaada yao, ambapo mwalimu alisema kuwa hawezi
kwenda nyumbani kwasababu anatokea mbali, hivyo akaamua kupumzika Kanisani na
mwenzake aliyekatwa mguu, ndipo usiku wakavamiwa
na kuawa Mwl huyo aliyekuwa anafundisha Kagemu sekondari, na aliyekuwa naye
kukatwa mguu ambaye ni Themistocres fundi selemara.
 |
Mchungaji FAUSTINE JOSEPH
Mchungaji CREODWARD EDWARD, ambaye ni mwenyekiti wa makanisa ya Kipentekoste amesema wanakaa kikao na wacvhungaji wote wa makanisa ya kikristo kutoa tamko kwasababu matukio ya namna hii yamekuwa yakitokea katika makanisa yao yasiyo yakawaida na yanawasikitisha sana. |
 |
Mchungaji CREODWARD EDWARD |
Polisi wamefika katika eneo hilo na kuondoka na mwili wa
marehemu pamoja na majeruhi, kwajili ya
kumpeleka hospitali, na inaelezwa kuwa amelazwa katika hospitali ya mkoa ambapo wachungaji wanakuta saa5 leo kutoa tamko. Tutakuletea undani wa taarifa hiyo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment