WANANCHI waliovamia Eneo la Nyantorotoro lililoko katika
kata ya Kalangalala wilayani Geita Mkoani humo, wametakiwa kuondoka mara moja
katika eneo hilo ili kumpisha muwekezaji mwenye leseni kuendeleza shughuli zake
za kuponda kokoto.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa madini wa mkoa wa Geita Eng.
Pius R. Lobe wakati akiongea na wananchi hao mara baada ya muwekezaji huyo
Majaliwa Maziku kulalamika kwa kusimama kwa shuguli zake baada ya wananchi wa
maeneo mbalimbali ya mji wa Geita kuvamia na kuanza kuponda kokoto katika eneo
lake.
Pius alisema kuwa mwekezaji huyo ana leseni kumi ambazo
zimesajililiwa kisheria na analipia mapato makubwa serikalini na kwamba wananchi
hao wanaoponda kokoto ni wavamizi wanatakiwa kuondoka mara moja kwani
walishalipwa mda mrefu lakini waligoma kuondoka kutokana na maneno ya baadhi ya
wanasiasa.
Jamani mnatakiwa kuondoka mara moja kwani mwekezaji huyo ana
leseni kisheria na mkiendelea kukaa hapa mtakamatwa na mtafikishwa mahakani
hatutaki kutumia nguvu, aliseama Pius.
Naye muwekezaji huyo Majali Maziku aliwatafutia Eneo lingine
wananchi hoa ili wasiendelee kuhangaika ila wengine walikwenda lakini wengine
waligoma jambo ambalo limemsababishia hasala kubwa kutokana na wavamizi hao
kuiba vifaa vya baadha ya mashine zake.
Wananchi hao walikubali kuondoka na kuongeza kuwa kumekuwa
na wanasiasa ambao wamekuwa wakiwachangisha pesa na kuwaambia kuwa mwekezaji
huyo hana haki kumbe ulikuwa na uongo na kumuomba mwekezaji huyo kuwapatia
ajira wananchi wa kijiji hicho.
Jamani tumekubali kuondoka kumbe tulidanganywa na viongozi
ambao si wazuri sisi tunakuomba utupatie ajirajapo tulikuchelewesha kufanya
kazi alisema Juma.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment