Kifo chake kimetokea siku chache baada ya
Zambia kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo.
Mwanasiasa huyo mkongwe aliingia madarakani
mwezi Septemba 2011 baada ya kuongoza chama chake cha Patriotic Front, na
kumshinda Rupiah Banda, ambaye alikuwa rais wakati huo na chama chake cha
Movement for Multi-Party Democracy, kikiwa madarakani kwa miaka ishirini.
Michael Chilufya Sata alizaliwa mwaka 1937
katika mji wa Mpika, eneo ambalo lilikuwa wakati huo ni Northern Rhodesia.
Muumini wa dini ya Kikristo ya madhehebu ya Katoliki, alifanya kazi kama afisa
polisi, mfanyakazi wa reli na mwanachama wa chama cha wafanyakazi wakati wa
utawala wa kikoloni. Baada ya Zambia kupata uhuru wake, pia aliishi kipindi
fulani mjini London, akiwa mfanyakazi wa reli, na kurejea Zambia, akiwa na
kampuni ya teksi.
Akiwa mwenye sauti ya mkwaruzo yakiwa ni
matokeo ya kuvuta sigara kwa muda mrefu, Bwana Sata aliibuka katika siasa na
kupata umaarufu katika miaka ya 1980.
Haraka akapata sifa ya kuwa gavana mwenye
kuchapa kazi kwa bidii, wakati akiongoza jimbo la Lusaka na mtu wa utekelezaji
kwa vitendo.
Lakini pia alijulikana kama mtu wa kutoa
amri, mtu asiyeendekeza urafiki na mkali- na wapinzani wake walisema jina
alilopewa la bandia la "King Cobra" alikuwa anastahili kuitwa hivyo.
Kwa mara ya kwanza alionekana kama mtu ambaye
angetekeleza ahadi za kupambana na rushwa na kupata ufumbuzi wa tatizo la ajira
na kuleta ustawi wa jamii. Lakini kipindi chake madarakani kiligubikwa na
kuuzima upinzani wa kisiasa na kudorora kwa uchumi.
Bwana Sata ni rais wa pili wa Zambia kufariki
dunia akiwa madarakani.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment