![]() |
| Baba askofu Kilaini akizungumza na mwandishi Mac Ngaiza, katika makaazi yake Bunena Bukoba mjini. |
“katika shughuli za kijamii, watu wanapotoka
katikabaadhi ya taratibu kuwa kitu Fulani kinazuiliwa lakini ngoja tufanye
kidogo, tofauti na dini inayoagiza kuwa hata kujaribu ni kosa, hayo ndiyo mambo
Mwalimu alizingatia” amesema Kilaini.
Amesema kuwa mambo yanayomsikitisha zaidi, ni
kuendelea kutumia jina lake kwa uongo huku mambo ambayo yalianzishwa naye
wakati huo yakichakaa na viongozi wakiendelea kuyatumiahuku yakiwaumiza
watanzania, akitolea mfano wa meli ya Mv Victoria,ambayo amesema mpaka sasa ina
zaidi ya miaka 60, hivyo imechakaa na inaendelea kuwasumbua watanzania hasa
wakaazi wa mkoani Kagera, ambao tangu awali waliamini usafriri huo na
uliwasaidia, lakini viongozi wameziba m,asikio kufanya utaratibu katikahilo.
Amesema melihiyo zamani ilikuwa ikifika ukoba sa 12
alfajiri kutokea Mwanza, lakini sasa anaisikia saa 3 asubuhi, kuwa hicho ni
kiashiria kuwa ina matatizo makubwa na ikiendelea kufanyiwa mzaha itapoteza
watanzania wengine katama ilivyotokea 1996.
Na Mwanaharakati.



No comments:
Post a Comment