Baada ya vyombo vya habari kuripoti
kuhusu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu na msanii wa filamu Aunty
Ezekiel kuvinjari nchini Marekani hatimaye waziri huyo atoa ufafanuzi.
Nyalandu alisema tuhuma hizo
zimetengenezwa na kundi la watu ambalo miongoni mwao ni baadhi ya viongozi wa
Serikali ambao humchafua kutokana na utendaji kazi wake.
Nyalandu alisema alikwenda Marekani
septemba12 kwa ajili ya kufungua tamasha la utamaduni na utalii kupitia soko la
wasanii wa Tanzania ambako alikutana na msanii huyo mara moja pamoja na
mwingine wa Bongo Fleva Kassim Mganga usiku katika moja ya maeneo nchini humo.
Alikana kutanua na msanii huyo kama
baadhi ya nyombo vya habari vilivyoripoti na kusema maneno hayo ni kwa lengo la
kumwaribia heshima yake mbele ya jamii.
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment