
![]() |
| Mama wa Mtoto akiwa hospital baada ya kuzimia. |
Akizungumza kwa uchungu, mama mzazi
wa mtoto huyo, Zakia Peter ambaye amelazwa katika Zahanati ya Kellen kutokana
na mshtuko wa kifo cha mwanaye, alisema siku ya tukio, hausigeli huyo aliyekuwa
na siku mbili tangu aanze kazi aling’ang’ania kutumwa sokoni saa mbili asubuhi
ambapo alimkubalia na kumuagiza mboga.
Mama wa marehemu aliendelea kusema
kuwa zoezi la kumsaka msichana huyo na mtoto wake liliendelea mpaka Jumanne
iliyopita ambapo habari zilisambaa kwamba kuna maiti ya mtoto wa kiume imekutwa
ikielea kwenye dimbwi la maji machafu linalotumika kumwagilia bustani za mboga
maeneo hayo.
mwili huo ulipelekwa katika
Hospitali Teule ya Tumbi, Kibaha ambapo madaktari waliufanyia uchunguzi na
kubaini kuwa marehemu alinyongwa shingo na kupigwa na kitu kizito kichwani hali
iliyomsababishia mauti.
Baadhi ya watu waliozungumza na
gazeti hili Jumatano iliyopita akiwemo mama wa marehemu, walisema kwa siku
mbili hizo alizofanya kazi hausigeli huyo alionekana kuwa na mambo ya kishirikina kwani asubuhi ya siku
ya tukio aliamka akiwa amenyolewa nywele upande mmoja.
“Siku hiyo ya Jumapili huyo mdada wa
kazi aliamka akiwa amenyolewa nywele upande mmoja, alipoambiwa amalizie zote
alikataa akisema atanyoa baada ya kutoka sokoni ambapo hakurudi tena,” alisema
mama wa marehemu.
Jumatatu iliyopita, siku moja baada
ya tukio, hausigeli huyo alikutwa akirandaranda stendi akiomba fedha za nauli
ili arudi kwao Mbeya lakini alikamatwa na kufikishwa kwenye kituo kidogo cha
polisi.
Habari zinasema hali kwenye kituo
hicho ilikuwa mbaya kufuatia baadhi ya wakazi wa eneo hilo kujaribu kukivamia
ili wamuue mtuhumiwa huyo. Ilibidi mtuhumiwa ahamishiwe Kituo cha Polisi cha
Tumbi, Kibaha
Na Mwanaharakati.


No comments:
Post a Comment