IKIWA ni siku chache tangu Ofisa
madini wa Mkoa wa Geita Eng Pius R. Lobe kuwaamuru wavamizi waliaovamia
eneo la Nyantorotoro kuondoka mara moja na kumpisha mwekezaji mwenye
leseni Majaliwa Maziku kufanya shuguli zake.
Kumezuka utata baada ya M/Kiti
wa CCM Mkoa wa Geita Joseph Msukuma kutajwa kuhamasisha wananchi kuvamia
eneo hilo tena kwa ajili ya kufanya fujo.
Jambo hilo la kushangaza na kusikitisha limetokea jana majira ya saa tano asubuhi ambapo M/Kiti alikwenda katika eneo hilo na wananchi wa kijiji hicho na kuanza kufanya fujo huku wakilazimishwa kuingia ndani ya eneo hilo wakidai hawajalipwa sitaiki zao.
Wafanyakazi wa mwekezaji waliokutwa
wakiendelea na kazi katika eneo hilo waliamua kutimua mbio mara baada ya
wananchi hao kuingia kwenye eneo hilo na kuendelea kuponda kokoto mpaka
watakapolipwa sitaiki zao.
“Jamani mimi kama M/Kiti wa CCM
nasema msiondoke katika eneo hili endelea kuponda kokoto mpaka mlipwe haki zenu
zote na hakuna wa kuwafukuza hata awe nani” alisema Msukuma.
Baada ya muda mfupi jeshi la polisi
likiongozwa na OCD wa Wilaya ya Silvester Ibrahim Geita walifika na kuamuru
wavamizi hao kuondoka mara moja kwa hiyari yao na walikubali kuondoka wao
pamoja na M/Kiti huyo.
Afisa Madini wa Mkoa wa Geita
Eng. Pius R. Lobe alisema kuwa wao wanafuata sheria inasema nini na si
wanasiasa na huyo M/Kiti anawanganya na atawaingiza matatani kwani watakamatwa
na kufikishwa mahakamani bila kujali nani wala nani. Na kuongeza kuwa hakuna
mtu yoyote anayedai, watu wate walishalipwa zamani na kutafutiwa eneo jingine.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Geita Omary
Manzie Mangochie aliwataka wananchi wa eneo hilo kuacha kusikiliza siasa za
kiongozi huyo bali wafuate sheria za nchi wasije wakaumia bure na kuacha
familia zao zikihangaika.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment