Mwanamuziki Nassib Abdul, ‘Diamond Platnumz’ amesalimisha
nguo zake za kijeshi kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

“Nisingeweza kukaidi amri ya dola, nilifika na yale mavazi
na nikahojiwa kwa saa kadhaa. Nikaeleza kwamba yalikuwa yakifanana na ya jeshi
na hayakuwa sare rasmi za jeshi hilo, kikubwa nilihitaji kumaliza tatizo,”
alisema nyota huyo aliyetajwa kuwania tuzo za MTV EMA zinazotarajiwa kufanyika
Novemba 9 mjini Glasgow, Scotland.
Diamond alisema si kweli kwamba alichukuliwa dhamana na
Chifu Kiumbe, ila ukweli ni kwamba alisindikizwa na mdau huyo wa sanaa nchini
kama kaka yake kutokana na woga aliokuwa nao, lakini hakushikiliwa na kutakiwa
dhamana yoyote.CHANZO BONGO CLAN
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment