WANCHI wa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza wamepongeza huduma inayoedelea kutolewa na benk ya CRDB kwa kuendelea kueneza huduma za ulipo tupo na Kuongeza ATM ili kupunguza usumbufu waliokuwa wakiupata.
Hayo yamebainishwa jana na baadhi ya
wananchi wa kijiji cha Kanyala katika Wilaya hiyo wakati benki hiyo
ilipokuwa ikifungua huduma hiyo katika kijiji hicho na kusambaza huduma ya
ulipo tupo kila kona.
Mwananchi mmoja ambaye ni
mfanyabishara wa samaki Juma Masanja alisema kuwa kuwekwa kwa huduma hiyo kwani
walikuwa wakihangaika sana kutunza pesa na kuchukua pesa lakini kuwekwa kwa
huduma hizo wananchi wataacha kusumbuka.
Aliongeza kuwa wagonjwa wengi
walikuwa wanahangaika pakutunzia pesa walikuwa wanatembea walikuwa wanatembea
zaidi ya kilomita 15 kutafuta huduma hiyo kwahiyo kuwekwa kwa huduma hiyo ni
mkombozi kwao.
Jamani tunashukuru benki hii kwa
kuweka huduma kama hii kalibu na wananchi kwani tulihangaika sana kwa sasa benk
ya CRDB Ni mkombozi wetu alisema.
Mkuu wa Wilaya hiyo Kareni Yunusu
alipoulizwa juu ya huduma hiyo kwa wananchi wake alisema kuwa alitoa pongezi
zake kubwa kwa benk hiyo na kuomba mabenki mengine kuiga mfano kama huo
wa CRDB.
Naye Meneja msimamizi katika Wilaya
hiyo ambaye ni Leonce Matley wa Mkoa wa Geita alisema wameamua
kutoa huduma hiyo kutokana na maombi ya wananchi wa kjijiji hicho na
wataenderea kushirikiana na wanachi kutoa huduma hiyo na watazidi
kupeleka vijijini zaidi kwani ndiko bado wananchi wanahangaika sana kuliko
mjini
Tuendelee kushirikiana sisi na ninyi
wananchi kwa kutoa huduma tunapokosea tunaomba mtuambie kwani tunataka
kutoa huduma iliyo bora na ukizingati biashara ni ushindani alisema
Matley.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment