Marehemu Sherry enzi za uhai wake
Kama kawa baada ya vituko hivyo
Mwandishi wa mtandao huu alimtafuta msemaji wa familia hiyo Kulwa Choka ambapo
alikiri kuwepo kwa vituko hivyo.
” Nikweli baba yetu mzee Choka yuko Tunduma hakuweza kufika kwenye msiba wa mwanae na kwamba amepiga simu nakumpa madalaka yote babu yetu mzee Msafiri Ngedele ndio maana unaona msiba uko hapa Mji Mpya nyumbani kwa mzee huyo, pia huyo mzee Magali ambaye watu wanadai ni baba yake Sherry pia hakufika msibani"alisema Kulwa kwa Jazba na kuongeza kusema
"kuhusu jina la kwenye msalaba tumekuwa na mvutano wa takribani masaa 4 kwenye kikao mama wa marehemu alitushangaza kuacha jina la baba wa marehemu mzee Choka na kung’ang’ania kuandika msalaba jina la baba yake mzee Msiba Edward ambaye ni babu wa dada yangu sherry kwa upande wa mama yake,tumeona tusiwape watu faida tumekubali lakini undani zaidi wa matukio hayo tutakujuza baada ya kumaliza msiba huu”alisema Kubwa Choka ambaye amechangia baba na marehemu Sherry.
Juhudi za Mtandao huu za kutaka kuzungumza na Mama mzazi wa Sherry Afande Flora Msiba zilikwama baada ya mama huyo muda wote kuangulia kilio kwa kuondokewa na mpendwa mtoto wake juhuzi hizo zinaendele leo na kesho,Pia juhuzi za Mwandishi wetu kumhoji mzee Choka kwa njia ya simu zinaendele,
Pekuapekua ya Mtandao huu imefanikiwakumbana mmoja wa wasanii nyota wa bongo Movie kutoka Dar ambapo alipoulizwa kwa nini mzee Mgali hakufika kwenye msiba wa Sherry alisema” Nikweli mzee magari hakufika kwenye msiba wa Sherry yuko Mwanza kwenye shughuli za kisanii”alisema msanii huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment