MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 26 October 2014

LUNDENGA AKANUSHA KUJIUZULU KWA MISS TANZANIA 2014

 

“Habari za jioni Watanzania wenzangu, kutokana na kuwa nimekuwa nikisemwa sana, maneno mengi yasio na tija juu ya hili taji la U-Miss anzania 2014,,mpaka kupelekea nisiwe na amani na uhuru ndani ya nchi yangu Tanzania, kwa roho safi nimeamua mwenyewe kujivua taji hilo na kuacha wanaye ona anastahili taji hili apewe ili niendelee na maisha yangu kwa amani ,isiwe shida sana kwani sitegemei taji hili ili kuishi!!” imeandikwa katika ukurasa huo.
Akizungumzia uvumi huo, Lundenga alisema hakuna ukweli juu ya taarifa hiyo, na kwamba kama lingekuwa na ukweli ni wazi kwamba Sitti angeiarifu kampuni yake, inayoratibu kinyang’anyiro hicho kilichotimiza miaka 20 mwaka huu.
“Hakuna taarifa iliyotufikia hadi sasa kuhusiana na taarifa hizo. Sitti anajua anapaswa kufanya nini kama anaamua kulitema taji, ambapo anapaswa kutuarifu sisi kabla ya kuripoti hilo mahali popote. Kwa kuwa hajafanya hivyo, tunaamini hilo halipo nab ado tunamtambua kuwa mrembo wetu,” alisema Lundenga.
Kwa upande wa mama wa mrembo huyo, alisema ameshtushwa na taarifa za mwanaye kujiuzulu na kusema si za kweli, kwani kama angepanga kufanya hivyo asingefanya kwa kificho, badala yake angeitisha mkutao na wanahabari: “Hawezi kujiuzulu kienyeji hivyo na hata mimi mama yake sina taarifa hizo, hayo ni matumizi mabaya ya mitandao.
 

Na Mwanaharakati.

No comments: