Katika hali ya kushangaza huku kila
mtu akifikiria yake baaya ya juzi huko mkoani Tabora, kutokea tukio la aina
yake ambapo inaelezwa kuwa mti aina ya Msufi uliokuwa umeanguka yapata miaka
mitatu iliyopita umesimama ghafla tena kwa sauti kubwa ya mrindimo na kuwafanya
wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo.

Tukio hilo limetokea Oktoba 17,mwaka
huu,katika kijiji cha Mfuto kata ya Ufuluma katika wilaya ya Uyuwi mkoani
Tabora.
Inaelezwa kuwa mti huo wenye kipenyo
cha futi 2 uliinuka na kuwa kama zamani baada ya kutokea upepo mkali katika
kijiji hicho.
Wananchi walikusanyika kila mmoja akitaka
kuchukua angalau gome la mti huo kwa ajili ya dawa ama kumbukumbu , na haya
ndio maajabu ya Tanzania. Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment