Mtiti huo ulioshuhudiwa na
wanahabari wetu ulijiri wikiendi iliyopita, maeneo hayo ya Mbagala ambapo Aisha
aliongozana na shemeji yake katika ofisi hizo na kuibua tafrani kubwa
iliyokusanya kadamnasi na kufunga mtaa kwa muda.
|
Aisha alipofika ofisini hapo
alishikwa na ghadhabu baada mhasibu wa kampuni hiyo kumwambia hakuwa na namba
ya bosi wake wakati alijua akifika tu angepewa fedha hizo hivyo akashikana naye
mashati na kuanza kuzipiga ambapo Aisha alisukumwa akadondoka pwaa!
Kitendo cha kusukumwa, kilimpandisha
hasira Aisha na kuamua kuchukua jiwe ambalo lilishindwa kufungua mlango hivyo
alichukua nondo na kuvunja mlango huo ambapo wafanyakazi walijifungia kwa ndani
ili kumzuia asiingie ndani.
Wanahabari wa gazeti hilo walipomfuata
Ngeze kujua kulikoni kumtia mbaroni Aisha alisema alivamiwa na staa huyo na
mabaunsa ambao walivunja ofisi pamoja na kushukua ‘laptop’ na fedha.
Mpaka kuchapisha taarifa hizi, Aisha
na shemeji yake walikuwa bado wameshikiliwa na Polisi wa Kituo cha Maturubai,
Mbagala.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment