Akizungumza nasi, Afisa Mtendaji wa
kata ya Mtindiro, Ester Kaima, alisema kuwa mkulima huyo aliuawa na watu hao na
kufungiwa ndani ya nyumba yake katika shamba la mmiliki wake Halidi Semboni.
Alisema baada ya watu kufanya mauaji
hayo walitokomea kusikojulikana.
Alisema mwili wa mkulima huyo
uligundulika siku ya tatu baadaye baada ya majirani kusikia harufu ikitoka
ndani ya nyumba hiyo.
Katika tukio jingine Salima Rashidi
amejiua kwa kunywa sumu.
Tukio hilo limetokea katika kijiji
cha Kwabada kata ya Mtindiro.
Jeshi la polisi wilayani Muheza
limedhibitisha kutokea matukio hayo.
Na Steve William
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment