Baadhi ya Polisi wa doria ya
Pikipiki wakiwa nje ya kiwanda cha Bora.
Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni
majambazi wamepora begi linalodaiwa kuwa na fedha kisha kumpiga risasi ya
shingo mwendesha boda boda na kupora pikipiki yake nje ya Kiwanda cha Bora,
barabara ya Nyerere Dar es Salaam.
Chazo kilifika eneo la tukio na
kukuta watu wakielezea tukio hilo na kulifananisha na la sinema kutokana na
kile walichokiona.
"Tuliona mzee mmoja tunahisi ni
mfakazi wa Bora, alifika na pikipiki hapa, wakati anataka kuingia ndani
wakafika watu wengine wawili katika pikipiki na kuamuru kupewa begi lile na
ghafla mwenda pikipiki akawa anawahoji inakuaje wanachukua begi hilo ndipo
tukasikia mlio wa risasi na bodaboda yule akaanguka chini wakamsukuma na
kuchukua pikipiki yake na kukimbia nayo," alisema shuhuda yule.
Polisi ilifika eneo la tukio huku
wengine wakiendelea na msako mkali dhidi ya wahalifu hao wakutumia sihala huku
hofu ya kijana yule wa boda boda kupoteza maisha ikiwa kubwa kutokana na eneo
alilopigwa risasi.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment