Wapanga mipango nchini wameaswa
kuzingatia weledi wakati wa kuandaa maandiko ya miradi yanayowasilishwa kwa
wafadhili ili kuongeza ushindani dhidi ya nchi nyingine wakati wa uwasilishaji
wa maombi ya kupatiwa ufadhili wa miradi ya maendeleo.
|
Kaimu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (aliyesimama) akizungumza na baadhi ya viongozi waandamizi wizara za viwanda na biashara, fedha, uchukuzi, nishati na madini pamoja na viongozi waandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Zanzibar. |
Pichani ni baadhi ya viongozi waliohudhuria Kikao hicho. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Dkt. Adelhelm Meru. |
Mmoja wa wajumbe wa kikao hicho, Bw.
Aunyisa Meena kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara akichangia mada.
Wito huo umetolewa na Kaimu Katibu
Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati
alipofanya mazungumzo na viongozi waandamizi kutoka wizara za viwanda na
biashara, fedha, uchukuzi, nishati na madini pamoja na viongozi waandamizi
kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Zanzibar.
Bibi Mwanri alisema kuwa kuna ushindani
mkubwa kwa nchi zinazoomba ufadhili wa miradi ya maendeleo hivyo uandishi wa
maandiko yenye kuzingatia weledi na viwango vya kimataifa ni msingi katika
kuongeza ushindani na kuweza kuwashawishi wafadhili kuvutiwa na miradi husika.
“Katika kukabiliana na ushindani hatuna
budi kujikita katika weledi na kuandika maandiko yenye kuweza kuvutia wafadhili
ili waweze kuja kuwekeza nchini kwetu, ili tuweze kutimiza ndoto zetu za
kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati kufikia mwaka 2025” alisema
Bibi Mwanri.
Mwezi Juni mwaka 2011, Serikali iliandaa
Mpango wa Kwanza wa Maeneleo (2011/12 – 2015/16) kwa lengo la kutekeleza Dira
ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambapo Mpango huu ulihitaji takribani trilioni 40
ili kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano.
Kwa mujibu wa Mpango huo, vyanzo vya
utekelezaji wake ni pamoja na Ubia Kati
ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP);
uwekezaji wa kigeni; Hati Fungani kwa Waishio Ughaibuni; Hatifungani za
ndani; Hati Fungani katika Masoko ya Nje; Mifuko ya Pensheni na hifadhi ya
jamii; na makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi wa nchi zinazoendelea.
Na Saidi Mkabakuli
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment