Gari Moja ya Kampuni ya Uchimbaji wa
Dhahabu Mkoani Geita (GGM) imekamatwa na wakala wa mahakama kuu Mwanza na
nyingine moja kukimbia baada ya kampuni hiyo kushindwa kulipa deni la zaidi ya
Sh.57milioni.
Gari hiyo aina ya Toyota Hiace yenye
namba za usajili T258 ilikamatwa jana majira ya saa 7:00 mchana wakati gari hilo
likiwa barabarani kueleka kazini huku dereva wa gari nyinyingine ambaye
hakujulikana mara moja kutokomea kusikojulikana baada ya kuwaona wakala
hao wakikamata gari hilo.
Taarifa zinasema kuwa GGM ilishindwa
kumlipa Peter Daudi kiasi hicho cha fedha ikiwa ni agizo la mahakama kuu
Mwanza iliyoitaka kampuni hiyo kumlipa stahiki zake baada ya
kushinda kesi namba 23 of 2014 iliyokuwa ikimkabili GGM kwa kumsimamisha kazi
kinyela kwa tuhuma za wizi wa Mafuta.
“Mimi nilikuwa mwajiliwa wa
GGM, nimefanya nao kazi kwa muda wa miaka mitano ,ilipofika mwezi wa nane
mwaka 2012 nilisimamishwa kazi”alisema Daudi
Daudi alieleza kuwa baada ya
kusimamishwa kazi aliamua kwenda mahakamani akisaidiwa na chama cha wafanyakazi
Mgodini (TAMICO) ambapo alishinda kesi na kutakiwa kurudishwa kazini na
kulipwa fedha zake zote za mshahara ndani ya siku 42 wakati akiwa nje ya
kazi.
“GGM ilishindwa kunilipa ikabidi
nirudi mahakamani kukazia hukumu,nikapata’ Court Broker’ wakala wa kukamata
mali ambao wamekamata magari gari moja na nyingine dereva amekimbia nayo
“alifafanua Daudi.
Pia Taarifa zinasema kuwa baada ya
gari ya GGM kukamatwa Kampuni hiyo iliamua kulipa sh.15 milioni kiasi ambacho
nikidogo na kwamba imelipa bila kufata utaratibu wa kimahakama huku kwani
imeingiza fedha hizo kwenye account ya Mwajiliwa huyo.
Hata hivyo msemaji wa kampuni hiyo
ambae ni meneja wa mawasiliano Tenga Tenga alipohojiwa juu ya tuhuma hizo
alisema kuwa hana taarifa hizo kwani yuko nje ya kazi na kuomba apewe
muda ili aweze kufatilia suala hilo kisha atolee majibu.
“Niko nje ya Kazi naomba nifatilia
alafu nitatoa majibu baadae baada ya kupata taarifa sahii toka ofisini”alisema
Tenga……..
Akizungumza na waandishi wa habari
katibu wa chama cha wafanyakazi Wilaya ya Geita (TAMICO), Paternus Rwechungura
ambaye alikuwa anasimamia kesi hiyo alithibitisha kuwepo kwa kesi hiyo na
kwamba mfanyakazi huyo alishinda kesi lakini GGM ikashindwa kulipa kwa muda wa
siku 42 walizopewa na mahakama .
Baada ya kushindwa kulipa kwa muda
huo aliamua kwenda kukazia mahakama na kesi hiyo ni meisimamai amimi mpaka leo
hii mali ya GGM imekamatwa na ukamataji huo umezingatia thamani ya fedha
anayodai.”alisema Rwechungula.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment