Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Bongo
anayekuja juu kwa kasi, Janet Mrema anayedaiwa kutoroshwa na mchungaji huyo.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mchungaji huyo alifika nyumbani kwa Jonas Mrema,
mume wa Janet, maeneo ya Tegeta-Nyaishozi jijini Dar na kuishi kama mtumishi wa
Mungu lakini polepole alianza mazoea tata na Janet.
“Mume alianza kuhisi mabadiliko ya
mkewe kwa mtumishi huyo, lakini nadhani aliona ni mawazo yake tu. Ndipo siku ya
siku akashangaa mkewe na mchungaji huyo wameondoka nyumbani hapo.
“Kwa sasa tangu tukio hilo litokee
ni miezi kama mitatu. Mume alihangaika sana kumtafuta mkewe hadi jana (Jumatatu
iliyopita) ndipo akampata wakiwa na mchungaji huyo kwenye nyumba moja ambako
walikuwa wakiishi pamoja,” kilisema chanzo chetu.

Katibu wa Chama cha Waimba Injili
Tanzania, Stela Joel akilizungumzia sakata hilo. Iliidaiwa kwamba, mchungaji
huyo alipopekuliwa alikutwa na paspoti ya nchini Burundi wakati yeye ni Mkongo
wa Uvira na alionekana kuishi nchini kinyume na sheria hivyo alifunguliwa
jalada la kesi kwenye Kituo cha Polisi cha Wazo Hili, Tegeta lenye Kumbukumbu
Na. WH/RB/7040/2014- KUISHI NCHINI BILA KIBALI.
Juzi, Amani liliwasiliana na Katibu
wa Chama cha Waimba Injili Tanzania, Stela Joel ambaye alikiri kutokea kwa
tukio hilo na kusema tayari chama hicho kimemsimamisha uanachana Janet kwa
kitendo chake hicho cha kumtoroka mumewe wa ndoa.
“Ni kweli na Chama cha Waimba Injili
Tanzania kimemsimamisha uanachama Janet. Hatuna mzaha katika maadili,” alisema
Stela.Amani lilimpigia simu mume wa Janet, Jonas Mrema ambapo katika mazungumzo
baada ya salamu alipewa pole kwa matatizo ya mkewe, alisema asante kisha
alipoulizwa kuhusu hali ilivyo aliomba apige simu yeye baadaye kwa vile alikuwa
kikaoni.
Hata hivyo, baada ya saa mbili
kupita bila kupiga, Amani lilimpigia tena simu ambapo iliita bila kupokelewa
hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.
No comments:
Post a Comment