Kiongozi wa Msafara huo, Bw. Wang Jianjun (Aliyesimama) ambaye ni Naibu Mkurugenzi Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji kutoka Tume ya Mipango na Maendeleo ya China akizungumza wakati wa ziara hiyo. |
Serikali imesema imedhamiria kuifanya
Tanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka wa fedha 206/2017 ili kuongeza kasi
ya kufikia lengo la Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambayo imedhamiria kuifikisha
Tanzania kuwa nchi yenye hadhi ya kipato cha kati na kuondokana na umaskini
kufikia mwaka 2025.
Akizungumza wakati wa kuwakaribisha
Ugeni kutoka Tume ya Mipango na Maendeleo ya China, Naibu Katibu Mtendaji
anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi, Bw. Paul
Sangawe, amesema kuwa Tanzania imedhamiria kuaandaa Mpango wa miaka mitano
utakaojikita katika uchumi wa viwanda ndani ya muda mfupi ujao.
“Tumedhamiria kuwekeza nguvu zetu kwenye
uwekezaji katika viwanda; katika Mpango wa Pili wa Maendeleo, nguvu kubwa
tunaiweka katika maendeleo ya viwanda ili kuweza kufikia malengo ya Dira ya
Taifa ya Maendeleo 2025,” alisema Bw. Sangawe.
Akizungumza wakati wa kikao cha pamoja
na viongozi wa Tume ya Mipango ya Tanzania, Kiongozi wa Msafara huo, Bw. Wang
Jianjun ambaye ni Naibu Mkurugenzi Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, alisema
kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi chache barani Afrika zenye fursa kubwa ya
kufikia maendeleo na kuweza kuondoka kwenye kundi la nchi maskini ndani ya
kipindi kifupi kijacho.
Bw. Jianjun aliongeza “ili kuweza
kufikia maendeleo ya haraka zaidi, ni vyema Tanzania ikaanza kuwekeza katika
viwanda hasa kwenye Maeneo Maalum ya Kiuchumi (SEZs) ili kuongeza tija katika
uzalishaji na kuongeza thamani bidhaa zake ili kuvutia masoko toka nje ya
nchi.”
No comments:
Post a Comment