MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday, 3 October 2014

NEWS ALERT!!! BALOZI KAGASHEKI UMUHIMU WA SHULE YA VIZIWI MUGEZA

Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Balozi Khamis Kagasheki akihutubia katika sherehe za kuhitimu darasa la saba kwa walemavu wa kutosikia( viziwi) Mugeza mjini Bukoba.

 Katika sherehe hiyo Kagasheki amempongeza mwalimu mkuu mstaafu Bwana Rutabingwa, huku akiwasihi walimu wengine kuiga mfano wake wa kuomba kufundisha katika shule hiyo kutokana na kuwa na kazi ngumu ya kufundisha watu wenye ulemavu wa namna hiyo.
Kutoka kushoto ni mwalimu mkuu mstaafumzee Rutabingwa, mwl Nicolaus Ishababi aliyeamishiwa Ndolage, Mh Kagasheki na mwalimu mkuu wa sasa.

Balozi Kagasheki kulia akiteta jambo na dokta wa masikio DC Amin

Walimu wa kigeni katika shule hiyo wakifuatilia hotuba ya mh Balozi.

Shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya vitendea kazi, uhaba wa walimu, na miundombinu hafifu kutokana na kuchakaa kwa ile iliyowekwa tangu awali, huku mbunge Kagasheki akisema kuwa yuko pamoja nao na ataendelea kuisaidia shule hiyo kama alivyokuwa akitoa hicho kidogo alichonacho.
Na Mwanaharakati.

No comments: