Ni baada ya matatizo yanayoisibu meli hiyo na kuzua wasiwasi kwa abiria, huku wakisisitiza rais kutimiza ahadi.
Baadhi
ya wabunge wa mkoani Kagera wameiomba serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi, kusimamisha
meli ya MV VICTORIA kuendelea na safari zake kati ya Mwanza na Bukoba mpaka
ifanyiwe matengenezo, au iletwe nyingine.
Akizungumza
kwa niaba ya wabunge hao, Mbunge wa jimbo la Muleba Kaskazini, CHARLES MWIJAGE
amesema kuwa haiwezekani kuona meli hiyo ambayo inatia shaka kuendelea
kusafirisha watu.
Bwana
Mwijage amewaomba wananchi kuwa wavumilivu, wakati wabunge
hao wakishirikiana katika kufuatilia ahadi ya rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Kikwete
ya kununua meli mpya.
Mwishoni
mwa wiki, abiria 381 waliokuwa
wanasafiri na meli ya MV Victoria, kutoka Bukoba kwenda Mwanza, walikumbwa na hofu baada ya mfumo wa
kuendesha meli hiyo kushindwa kufanya
kazi ikiwa majini.
Meli
hiyo iliyoondoka katika bandari ya Bukoba Ijumaa usiku, mfuko wake wa kuendeshea meli ulishindwa,
ikiwa zimebakia maili kadhaa kabla ya kufika katika bandari ya Kemondo.
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment