Jana kumesambaa tetesi kuwa kuna uwapo wa mgonjwa wa Ebola katika hospitali ya mkoa, jambo ambalo limewapa wasiwasi wananchi katika viunga vya mji wa Bukoba, ambapo MAC MEDIA imefanya jitiada za kuupata uongozi wa mkoa kuzungumzia jambo hilo kiundani bila mafanikio, japo hakuna taarifa rasmi za ugonjwa huo mkoani Kagera.
Kutokana na uchunguziuliofanywa na MAC MEDIA imebainika kuwa kulikuwa na zoezi la kupima juhudi zinazoweza kuchukuliwa kama akijitokeza mgonjwa wa Ebola mkoani Kagera ili ijulikane wanaweza kusaidia na kujikinga je.
Taarifa za baadhi ya wafanyakazi katika hospitali hiyo waliotudokeza kwa masharti ya kutokutajwa majina,wamesemaaliletwa mgonjwa ambaye alijifanya kuwa na dalili za ugonjwa huo, hukuikisemekana kuwa ametokea nchini Uganda, na uongozi wa hospitali ukafunga baadhi ya maeneo ya hospitali hiyo ili kumuudumia mgonjwa huyo na badaye utaratibu huoulimalizika kimya kimya, huku wananchi Bukoba wakisalia wasiwasi ya kuogopa kufika hospitalini hapo
Na Mwanaharakati.


No comments:
Post a Comment