WANANCHI
wameshauriwa kuisoma Katiba Mpya Inayopendekezwa sura kwa sura na ibara
kwa ibara ili waweze kupata uelewa wa masuala mbalimbali yaliyomo ndani ya
Katiba hiyo na kuacha kusikiliza maneno ya watu yenye nia ya kupotosha
ukweli.
Kauli
hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.
Asha Rose Migiro wakati wa sherehe za mahafali ya pili ya
Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira
hatarishi ya WAMA Nakayama, iliyopo wilayani Rufiji
mkoani Pwani.
Dkt
. Migiro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo,
ambayo ilihudhuriwa na baadhi ya viongozi , wakiwemo baadhi ya wake
za viongozi na wageni wengine mbalimbali.
“Nchi
yetu ilikuwa katika mchakato wa uandikaji wa Katiba Inayopendekezwa kazi
ambayo ilikamilika Oktoba 8, mwaka huu.
kazi
iliyombele yenu ni kuisoma Katiba hii sura kwa sura ibara kwa
ibara.
"Tusikubali
kusomewa na tutakapokamilisha kazi ya kuisoma tuipigie kura ya ndiyo,”
alisema Dkt. Migiro.
Akizungumza
na katika mkutano wa mabalozi wanazoziwakilisha nchi zao katika Jamhuri ya Watu
wa China uliofanyika kwenye Nyumba ya kufikia Wageni ya Serikali ya Diaoyutai,
Beijing, Rais wa Jakaya Kikwete alisema Kura ya Maoni inatarajiwa kupigwa
wakati wowote Aprili mwaka ujao kama mambo yataenda vizuri.
Rais
Kikwete alikabidhiwa Katiba hiyo hivi karibuni mjini Dodoma baada ya Bunge
Maalum la Katiba kumalizia kaze yake.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment