Serikali
Tatu zingekuwa kejeli kwa Mwalimu Nyerere – Rais
.
Katiba Inayopendekezwa ndiyo hasa Katiba ya Wananchi
.
Siyo tu kwamba ni nzuri bali ni Katiba bora
![]() |
Kiongozi wa mbio za mwenge 2014 Rachel Kassandra akikabidhi mwenge wa Uhuru kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge ulius na kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora leo.Kulia ni Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na michezo Dkt.Fenela Mkangara. |
![]() |
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa
hotuba yake wakati wa kilele cha mbio za mwenge 2014 ziilizofanyika katika
uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora leo.
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema
kuwa sherehe za Kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, zingekuwa
zinamkejeli moja kwa moja Mwalimu kama Katiba Inayopendekezwa ingekubali
pendekezo la Serikali Tatu.
Aidha,
Rais Kikwete amesema kuwa hajui Watanzania wangesema nini katika sherehe za
mwaka huu wa Kumbukumbu hiyo kama Tanzania ingekuwa na Katiba Inayopendekezwa ingekuwa
imesisitiza Muungano wa muundo wa Serikali tatu.
Vile
vile, Rais Kikwete amesema kuwa Muungano wa Serikali Mbili ndiyo hasa urithi
mkuu ambao Mwalimu Nyerere aliwaachia Watanzania na wana budi kuendelea
kuulinda na kuuthamini urithi huo.
Rais
Kikwete alikuwa anazungumza na Taifa leo, Jumanne, Oktoba 14, 2014, kwenye
Sherehe ya Kuzima Mwenge wa Uhuru, Kumbumbuku za Mwalimu Nyerere na Kumalizika
kwa Wiki ya Vijana iliyofanyika kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora
ambao ulijaa maelfu kwa maelfu ya wananchi kuasdhimisha matukio hayo.
Rais
Kikwete amewaambia wananchi kuwa ni jambo mwafaka na faraja kabisa kuwa Katiba
Inayopendekezwa imesisitiza ubora wa
kuendelea na Muungano wa Serikali mbili alizoziasisi Mwalimu Julius Nyerere
akiwa na Mzee Abeid Amani Karume.
Amesema
Rais Kikwete: “Bila shaka mtakumbuka jinsi Mwalimu alivyoupigania muundo huu
kwa nguvu zake zote wakati wa uhai wake. Hatuna budi kulipongeza Bunge Maalum la
Katiba kwa kumuenzi kwa dhati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kudumisha
urithi wake mkuu.”
Ameongeza
Rais Kikwete: “ Sijui tungesema nini katika Sherehe za mwaka huu kama ndiyo
tungekuwa na Katiba Inayopendekezwa yenye Muungano wa muundo wa Serikali Tatu?”
“Sherehe
za mwaka huu ni spesheli kweli kweli kwani zinafanyika siku chache baada ya
Bunge Maalum la Katiba kukamilisha kazi na kukabidhi Katiba Inayopendekezwa,
Katiba ambayo siyo tu ni nzuri lakini ni Katiba bora. Nimebahatika kuisoma
Katiba Inayopendekezwa na naendelea kuisoma kwa sababu ina mambo mengi mazuri.
Kwa kweli ni Katiba bora kuliko hii tuliyonayo sasa yaani Katika ya Mwaka
1977.”
Amesisitiza
Rais Kikwete: “Hii ndiyo yenyewe hasa. Hii ndiyo Katiba ya Wananchi. Ni Katiba
inayotambua na kuimarisha tunu za taifa letu na mambo mazuri ya huko tulikotoka
na hapa tulipo. Ni katiba inayorekebisha upungufu uliopo sasa na kuweka mifumo
mizuri inayoendana na wakati tulionao sasa
na huko mbele tuendako. Kwa lugha nyepesi ni Katiba inayojibu changamoto
zetu za leo na kesho.”
Amewaambia
wananchi Rais Kikwete: “Katiba Inayopendekezwa inatokana na ushirikishwaji
mpana wa wananchi wa Tanzania walioko ndani na nje ya nchi. Hata Watanzania
waishio nje ya nchi walikuwa na uwakilishi ndani ya Bunge Maalum la Katiba.
Ndiyo maana haki na maslahi ya makundi yote yametambuliwa na kupewa nafasi yake
stahiki.”
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment