Nyakiringa Stivin (39), mara baada ya kupigwa risasi tumboni. Kushoto kwake ni mkewe, Agness Lucas. |
Wapita njiawakijaribu kutoa msaada
kwa mtu huyo mwanamme aliyepigwa risasi maeneo ya Magomeni Mikumi ambaye
hakuweza kutambulika mara moja, lakini sasa amejulikana na kwa taarifa
zilizotolewa na ndugu, jamaa huyo amefariki dunia leo afajiri akiwa Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili.
Marehemu ametambulika kwa jina la
Nyakiringa Stivin (39), mkazi wa Kibaha Picha ya Ndege na mwanamke aliyekuwa
naye kwenye gari ameelezwa kuwa ni mkewe, Agness Lucas. Marehemu ni fundi wa
sofa na imeelezwa na chanzo chetu kuwa alikuja jijini Dar kwa ajili ya kununua
mahitaji yake ya ufundi.
Alipopigwa risasi maeneo ya Magomeni
alikuwa akitokea Access Bank Manzese ambako alitoa fedha kiasi cha shilingi
12M. Kwa mujibu wa mkewe, mkoba uliochukuliwa na majambazi ulikuwa na shilingi
milioni 10 ambazo zilibaki baada ya kufanya manunuzi maeneo ya Manzese.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment