Chanjo ya Surua
na Rubella kwa watoto, kuanzia miezi tisa hadi miaka 15 nchini kote limeanza
leo katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma ya afya.

Mratibu wa
Chanjo Mkoa wa Kagera, DEOCLES MJWAHUZI amesema
kuwa mwaka 2013 Watoto Elfu 72
na 611 walitegemewa kupata chanjo hiyo, lakini watoto waliochanjwa ni watoto elfu 35 na 979, ambapo ni pungufu na matarajio.
Amesema kuwa ili
kufikia malengo ya idadi inayotakiwa kuchanjwa na kuepusha tatizo la mwaka
jana, wazazi na walezi wote wenye watoto kuanzia miezi tisa hadi miaka 15 wanatakiwa kupeleka watoto wao ili
kupatiwa chanjo hiyo.
Ameongeza kuwa
katika chanjo hiyo, watoto laki
nne na elfu 71 na 214 watapatiwa dawa ya
Vitamin A ambapo watoto laki nne na elfu 18 na
857 watapatiwa dawa ya minyoo.
Bwana
MJWAHUZI amesema watoto
watakaochanjwa watakuwa na alama ya muda kwenye kidole kidogo cha mkono wa
kushoto, na kuwa watoto ambao hatakuwa na alama hiyo wazazi na walezi wao
watachukuliwa hatua za kisheria.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment