Mbongo Fleva, Judith Wambura Mbibo
‘Lady Jaydee’. Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, wawili hao walidaiwa kufikia
uamuzi wa kuvunja mkataba baada ya kuona ndoa yao inasuasua kutokana na
migogoro.
![]() |
Lady Jaydee’ na Gardner G. Habash ‘Kaptaini’ wakati wakiwa pamoja. |
Lady Jaydee au Jide alipoona mambo
yanakwenda ndivyosivyo alimshauri Gardner wavunje mkataba wa
Nyumbani Lounge ili kila mmoja awe na businesses (biashara) zake. “Walimfuata
mmiliki wa jengo, wakamwambia kwamba wanavunja, akawakubalia,” kilinyetisha
chanzo makini. Chanzo hicho kilizidi kwenda mbali zaidi na kudai kuwa mgahawa
huo kwa sasa unamilikiwa na mzungu.
“Mgahawa kwa sasa unamilikiwa na
Mzungu mmoja ambaye amenunua baadhi ya vitendea kazi walivyokuwa wakivitumia na
Jaydee amekuwa akimsaidia mzungu huyo baadhi ya mambo kwa kuwa ni mgeni Bongo
ila sasa Nyumbani Lounge itafunguliwa kwa jina jipya la M.O.G na Jaydee
atafanya shoo ya ufunguzi kama msanii tu,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kushibishwa maelezo hayo,
mwanahabari wetu alimtafuta Jide bila mafanikio lakini Gardner alipopatikana,
alijibu kwa kifupi.
“Siwezi kuzungumza chochote katika
suala hilo.”
Jide na Gardner wanadaiwa kutengana
na kila mmoja akiishi kivyake lakini wenyewe wamekuwa wakikanusha.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment