Mtu mmoja
anasemekana kupoteza maisha na mwingine kujeruhiwa baada ya Magari Mawili
waliyokuwa wanaendesha kugongana uso kwa uso katika eneo la Trans Oil kata ya
Nyasubi Wilayani Kahama mkoani Shinyanga usiku huu.
Tukio hilo
limetokea majira ya saa mbili usiku huu likihusisha gari aina ya Coster mali ya
Kampuni ya CK Safari Tours yenye namba T-468-CAL kugongana na Semi Teller aina
ya Scania yenye namba T-498-BVH.
Kwa mujibu
wa Mashuhuda, gari aina ya Coster ilikuwa ikitokea eneo la kituo cha Mafuta
kwenda Phantom, huku Scania hiyo ikitokea jijini Dar-es-salaam kwenda nchi
jirani na ndipo zikagongana uso kwa uso.
Taarifa
zinasema Dereva wa Scania hiyo ndiye huenda amefariki dunia huku dereva wa
Coster hiyo akisemekana kujeruhiwa na kupelekwa katika hospitali ya wilaya ya
Kahama kwa matibabu.
Chanzo cha
ajali hiyo bado hakijafahamika, na tayari Jeshi la polisi wilayani Kahama
limefika katika eneo la tukio na taratibu za kuyatoa magari hayo katikati ya
barabara zinaendelea.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment