Mdahalo uliokuwa ukifanyika katika
ukumbi wa Ubungo Plaza jijini DSM umeshindwa kuendelea kutokana na vurugu
zilizojitokeza ukumbini hapo.
Mdahalo huo uliokuwa unahusu Elimu
juu ya Katiba Inayopendekezwa ulikuwa umeandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere
na kushirikisha waliokuwa makamishna wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
wakiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji mstaafu Joseph warioba.
Jaji warioba ndiye aliyekuwa wa
kwanza kuichambua Katiba inayopendekezwa, na kuelezea mapungufu kadhaa ikiwa ni
pamoja na masuala ambayo Bunge La Katiba limeyaacha kutoka katika Rasimu ya
Katiba iliyoandaliwa na Tume hiyo.
Katika maelezo yake, Jaji Warioba
ameeleza kusikitishwa kwake na kuachwa kwa mambo ya muhimu ikiwa ni pamoja na
miiko ya uongozi pamoja na Tunu za Taifa, lakini amepongeza baadhi ya mambo
kuboreshwa ikiwa ni pamoja na Haki za Binadamu.
Wakati akielezea umuhimu wa kuweka
miiko ya uongozi kwenye Katiba, ndipo baadhi ya vijana wakatoa mabango yenye
ujumbe wa kupinga hotuba ya Warioba na kuunga mkono katiba
inayopendekezwa.
Bango mojawapo lilisomeka
“TUMEIPOKEA, TUNAIKUBALI NA TUNAIUNGA MKONO KATIBA PENDEKEZWA”
Baada ya hapo kilichofuata ni vurugu
zilizoambatana na mapigano miongoni mwao kati ya wanaounga mkono katiba na
wanaopinga.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment