MSANII wa vichekesho (komedy) kutoka Nigeria,Okopcha
Bright Onyekere maarufu kama Basket Mouth amewasifu wasanii wa Tanzania kwa
juhudi wanazofanya kuelimisha jamii kutumia vipaji vyao.
Akizungumza Dar es Salaam jana baada ya kuwasili
kutoka Nigeria kwa ajili ya onesho maalum kushirikiana na wasanii wa Tanzania
juzi Dar es Salaam alisema kutoka aanze sanaa ya vichekesho miaka 16 iliyopita
amekuwa akipata sifa za wasanii wa Tanzania wakiwika katika fani za muziki,
sanaa za filamu, michezo ya kuigiza na vichekesho.
Onyekere aliyetamba nchini Nigeria na Bara la Afrika
katika fani hiyo amekuja kufanya onesho moja lililopangwa kufanyika jana hoteli
ya Golden Tulip, aliongeza kuwa sanaa ni utajiri mkubwa kama vipaji walivyopewa
vitatumika ipasavyo na kutawala jukwaa .
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vuvuzela, Evans Bukuku
alisema lengo la kumleta msanii huyo wa komedy ni kuimarisha sanaa ya
vichekesho kwa wasanii chipukizi wa Tanzania ambao wanahitaji kuandaliwa kwa
soko hilo nchini na nje ya nchi.
Alisema Kampuni ya Vuvuzela imejitolea kusaidia
wasanii wa vichekesho nchini na kuwafundisha namna watakavyoweza kuendeleza
fani hiyo kazi iliyoanza miaka minne iliyopita kampuni ilipoanzishwa.
Bukuku alisema kila mwisho wa mwezi kuna onesho maalum
ambalo hutumika kuonesha vipaji vya wasanii wa vichekesho na jinsi msanii
anavyoweza kutawala jukwaa kuwaburudisha watazamaji.
Alisema kampuni yake inatarajia kufanya maonesho kama
hayo mikoa mbalimbali ya Tanzania kuibua wasanii wengine wenye uwezio katika
fani hiyo.
Mkurugenzi Bukuku alisema katika onesho la karibuni
Watanzania walikongwa nyoyo zao pale wasanii wa Tanzania washirikiana na
wasanii wa vichekesho kutoka Kenya ambaye ni Mdomo Baggy na Dick Omondi kutoka
Uganda anayejulikana kama Uncle Bob kufanya onesho kali nchini.
Bukuku aliwashukuru wadhamini waliojitokeza kusaidia
kufanyika kwa onesho hilo ambao ni Shirika la Ndege la Afrika Kusini
(SAA),Hoteli ya Golden Tulip, Gazeti la Mwananchi Communications, Clouds
Media Group, Ultimate security, Simu TV, Prime Advertising, Dar insites,
Advertising Dar, Bongo 5, Eventlites, Hugo Domingo na Michuzi Blog.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment