Na
Valence Robert Geita.
28.11.2014.
WAWEKEZAJI Mkoani Geita
wametakiwa kuwekeza kwa wingi kwenye Mkoa huo ili
vijana walioko kuweza kupata ajira kuliko kwenda kuwekeza kwingine
na kuwanufaisha wasiokuwa wazawa wa Mkoa husika.
Kauli hiyo imetolewa jana na
Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangochie wakati wa kufungua KG Hotell iliyoko
katika mtaa wa misheni kata ya kalangalala Wiyani Geita Mkoani hapa
iliyojengwa na mfanyabiashara mzawa.
Mangochie alisema kuwa
wafanyabiashara Mkoani Geita wamekuwa wakienda kuwekeza Mikoa mingine au
nchi za nje na kuwanyima haki ya kupata ajira vijana wazawa hivyo kuwaomba
kuendelea kuwekeza katika mkoa huwo ili na maendeleo yazidi kukua kwa kasi.
Jamani nawaomba
wafanyabishara wa Mkoa huu muwekeze katika Mkoa huu ili vijana wetu waweze
kupata ajira kuliko kuwekeza kwingine na ninawaomba kuzingatia kama kazi uliyo
nayo inaweza kufanywa na watu wa Mkoa huu sioni haja ya kwenda kutafuta
kwingine maana kuwapa ajira wazawa nanyi mnaongezewa zaidi alisema Mgochie.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment