Mwenyekiti wa bunge hilo IDD AZAN ZUNGU, amesema kuwa kiti cha SPIKA wa bunge hilo hakijapokea taarifa yoyote ya zuio kutoka mahakamani, hivyo kutokana na miongozo iliyotolewa leo na wabunge wakitaka kujadiliwa kwa sakata hilo, zitajibiwa jioni bungeni, huku akisema kuwa wabunge wasiwe na jazba kwani wapo kwa mujibu wa sheria.
Katika mkutano wa bunge hilo jana, Spika ANNE MAKINDA, alisema kuwa bunge haliwezi kusimamishwa na mahakama kufanya shughuli zake, hivyo kama kuna umuhimu, ni lazima taarifa ya ESCROW ijadiliwe bungeni.
Mh MAKINDA alisema hivyo baada ya wabunge kupokea taarifa ya mahakama kwa njia tofauti zisizo rasmi kuhusu zuio la mahakama kuwa bunge lisijadili suala hilo mpaka hatua kadhaa zitakapokamilika kisheria.
Bunge litaendelea leo jioni, na agenda ESCROW imeaidiwa kujadiliwa kwani hakuna taarifa rasmi ya mahakama kuzuia mj
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment